Nafasi ya Wazi ya Ajira: MADEREVA
Kampuni: GIN INVESTMENT LIMITED
Mahali: DAR ES SALAAM NA MWANZA – TANZANIA
Nafasi: 3 (DSM) & 2 (MWZ)
Kuhusu Sisi: GIN INVESTMENT LTD ni Kampuni binafsi ya Usimamizi wa Taka yenye leseni ya Manispaa ya kukusanya Taka ngumu na ada za usafi wa Mazingira kutoka kwa Mashirika ya Serikali na yasiyo ya serikali, Balozi, Kaya, Taasisi za kibinafsi na biashara
Majukumu Muhimu:
- Kuendesha magari ya Kampuni kwa ufanisi na usalama
- Kufanya ukaguzi wa gari kabla na baada ya kazi na kutoa taarifa ya haraka ya matengenezo ya gari kwa Msimamizi wako
- Kufuata kwa umakini sheria zote za barabarani, kanuni za usalama na sheria za Kampuni
- Kuwakilisha kampuni kwa ustaarabu katika mawasiliano yeyote na wateja
- Kuhakikisha vifaa muhimu vya gari kama spare tyre, kadi ya gari, fire extinguisher, jeki/toolbox vinatunzwa vizuri
- Kujaza logsheet kila trip au safari
Sifa:
- Barua ya maombi
- Wasifu wako wa kisasa (CV)
- Leseni ya Udereva ya Tanzania; Madaraja C na E
- Uzoefu usiopungua miaka 5 ya udereva kitaalam
- Nakala ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
- Cheti halali cha Udereva kutoka VETA / NIT
- Uthibitisho wazi wa leseni ya udereva kutoka Traffic Police
- Uwezo wa kufanya kazi kwa kujitegemea na kama sehemu ya timu.
Jinsi ya Kuomba: Waombaji wenye nia na wanaokidhi vigezo wanaalikwa kufika wakiwa nakala ya barua/ wasifu wake/ TIN na vyeti.
Usahili Utafanyika:
- Dar es Salaam ni siku ya Jumamosi tarehe 07/03/2026 - Kituo cha Mafuta Oryx – Victoria, Saa Kumi na Mbili na nusu Asubuhi
- Mwanza Ofisi ya GIN Investment; siku ya Alhamisi tarehe 12/03/2026 Saa Kumi na Mbili na Nusu Asubuhi.
Note: Interview Itafanyika siku hiyohiyo.